Mtalam III Mtalam III Author
Title: The Intro: Monstar, msanii mpya wa Bongo flava
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
The Intro inawalenga zaidi watu tofauti tofauti wanaochipukia kwenye fani mbalimbali kwa lengo la kuwapa exposure kwa wadau wa fani husika...
The Intro inawalenga zaidi watu tofauti tofauti wanaochipukia kwenye fani mbalimbali kwa lengo la kuwapa exposure kwa wadau wa fani husika. Hapa tunazungumzia muziki, filamu, modelling na fani zingine kwenye entertainment industry. Category hii itakuwa inawekwa kila Jumanne.
Leo kwenye The Intro tunamwangalia Monstar, msanii mpya wa Bongo flava ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo cha TIA hapa Dar es Salaam. Kupitia Interview hii hapa utaweza kujua historia yake kimuziki na nyimbo/video zake ambazo ameshazifanya:

Apart from music unafanya kitu gani? Student wa chuo gani au mfanyakazi wa wapi?
Mimi ni mwanafunzi nasoma degree katika chuo cha uhasibu (Tanzania Institute Of Accountancy) nko mwaka wa tatu sasa hivi. Nashukuru mwenyezi MUNGU naweza kumaintain muziki pamoja na shule kwan vyote naona vinaenda sawa.

Jina lako halisi unaitwa nani? 
Jina langu halisi naitwa Simon Sadala, ni msanii wa muziki wa bongofleva. Jina la sanaa najulikana kama Monstar.

Nani kaku-inspire kufanya muziki hapa Bongo na nje!?
Naweza kusema mtu ambaye amenispire kwa kiasi kikubwa kuingia katika game ni Q-Chillah, pamoja na Dully. Mzazi Keezy, hawa watu nawaelewa sana and i wish one day nifanye nao kazi inshallaah mwenyezi Mungu atajalia. Kwa nje ya nchi nawaelewa sana P Square, nipo na dream za kufika kama wao walipo sasa hivi.

Mtiririko wa kazi zako za muziki ukoje? Umefanya ngoma ipi na ipi mwaka gani na umefanya na music prod. ipi na wasanii gani na mwaka gani?
Nakumbuka kazi yangu ya kwanza kabisa niliifanya nikiwa mdogo sana ilikuwa mwaka 2006 pale kwa producer Nas lakini ngoma hiyo sikufanikiwa kuipeleka redioni. Mpaka sasa nimesharekodi nyimbo 6 timamu kati ya hizo moja ni video. 

Tracks ambazo zimeshaenda kwenye media ni pamoja na NITUNZIE nilioifanya pale Bokazy Ent, ambayo nilimshirikisha YAKI. Na ya pili inaitwa SIJAWASUSA hii niliifanya Expensive Music, zamani Usanii Prod. chini ya Producer Zidady Mwamba. 


Ngoma ya 3 ambayo ipo hewani kwa sasa inaitwa NIMEFIKA (watch here) nimeshirikiana na Big Jay P pamoja na Jim Jay pia nimeifanya apoapo Expensive Music. Nimefanikiwa kuzisambaza kadri ya uwezo wangu hasa ukizingatia usambaji umekuwa mgumu hasa kwa sisi wasanii tunaochipukia.


Unapata ugumu gani as an underground artist kwenye muziki wa Bongoflava?
Ugumu upo hasa kwenye mtaji linapokuja swala la kurekodi Audio na Video pamoja na swala la usambazaji wa kazi zangu hasa ukizingatia nafanya kila kitu kutokana na juhudi zangu mwenyewe ila ntafurahi sana kama ntapata management nzuri itakayosimamia kazi zangu.

Unatoa nafasi gani kwa mtu atakayetaka kukusponsor kimuziki?
Nakaribisha sana wadau mbalimbali waweze kunisapoti kwa hili ninalolifanya kwani naamin nna kipaji cha hali ya juu kuweza kusukuma muziki wetu mbele.

Watu gani ungependa kuwashukuru kwa kukufikisha hapo ulipo?
Kwanza napenda kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kunisaidia kufika adi apa ambako nipo leo hii, pili ni familia yangu kwa kuelewa ninachokifanya, tatu kwa mashabiki na  wadau mbalimbali wanaosapoti muziki wangu bila kuwasahau Keezy, Tbway360, Big JayP Tz, Jim Jay na wengine wote ambao sijawataja kwa majina, tuko pamoja sana endeleeni kusapoti Monstar a.k.a New Tone of Love.

Kitu gani kikubwa ambacho umefanya mpaka sasa kupitia muziki ambacho hutakisahau? Show/Music/Interview etc?
Kitu ambacho naweza kusema ni kikubwa kwangu ni kuwekwa kwenye jukwaa moja na mkongwe kwenye game kaka Dudubaya iyo ilikua mwaka 2011 kwenye event ya kusherekea sikukuu ya Christmass, Naweza kusema hii ni show ambayo watu walinielewa sana. Pia event nyingine ni interview yangu wakati natambulisha video yangu ya NIMEFIKA pale EATV salute sana kwa Tbway360.

Upo kwenye mitandao gani ya kijamii ukiacha huu wa Twitter? Weka link zake!!!
Napatikana kwenye mitandao hii ya kijamii
Facebook: Monstar Simon
Twitter: @monstar_simon
Instagram: @monstarsimon
WhatsApp: 0718-529001

Una lolote la kuongeza kuhusu unachokifanya ukiacha maswali nilokuuliza?   
Naomba wadau mbalimbali wa muziki waweze kunisapoti katika kazi zangu na pia kitu cha mwisho natoa ushauri kwa media mbalimbali ziweze kusapoti muziki wa nyumbani hasa kwa sisi flava mpya katika mziki huu wa bongoflava.

Download au Sikiliza moja kati ya nyimbo za Monstar hapa:


Endelea kutembelea mtandao wa keezywear kila Jumanne kwa ajili ya The Intro na share na wengine ili kuwainua undergrounds ambao wana uwezo waweze kusikika na kukuzwa.



Kama unataka kutokea kwenye category hii ya The Intro, tuma historia yako (katika mtindo huo wa juu) ya unachokifanya (Muziki, filamu, modelling n.k) kwenye email hii: keezywear@gmail.com

Usisahau kutuma na picha zako (si chini ya nne), contacts na link za akaunti zako za mitandao ya kijamii.

Author

Advertisement

 
Top