Chanzo kinasemekana ni yeye (Wema) kutokuwa na kawaida ya kuhudhuria misiba ya watu wengine. Akizungumzia ishu hiyo ya kususiwa msiba wa baba yake Wema alisema:
“Nimesikitishwa na kitendo hicho. Nahisi siyo sahihi kwa kuwa nimekuwa nikihudhuria misiba ya watu mbalimbali.
Hawakuwa sahihi kunifanyia hivyo katika kipindi hiki kigumu, hata hivyo, wangekuja kwanza tumzike baba ndiyo nijifunze ila kutokuja kwao hakujanipunguzia chochote.”
Kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa ni kama kumuongezea machozi mara mbili kwani tayari alikuwa na chozi la kuondokewa na baba yake kipenzi na la pili likawa ni kususiwa msiba.