Nyota wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa filamu yake aliyoitoa kumuenzi marehemu Steven Kanumba iitwayo After Death ilimlostisha kwa kuwa ilimpatia hasara kubwa.
“Nilitengeneza ile filamu kwa hela nyingi kidogo, kama milioni 35 au 40, nikafanya na uzinduzi pale Leaders Club uliogharimu kama milioni 13 hivi, lakini nilipokwenda kwa Wahindi wakanipa shilingi milioni 25, yaani inakatisha sana tamaa,” alisema muigizaji huyo wakati alipofanya mahojiano maalum aliyoyafanya na mwandishi wa Global publishers hivi karibuni.
Matangazo | Click them for more details:
• Tablet aina ya ‘Swag Tab - Expert 102’ Inauzwa kwa bei nafuu• Simu aina ya ‘Nokia N9’ Inauzwa kwa bei nafuu