Msanii wa filamu nchini, Shamsa Ford amesema kuwa yuko tayari kubeba ujauzito wa mpenzi wake, Nay Wa Mitego endapo wawili hao watakubaliana kupata mtoto. Baada ya kukiri kuwa kwenye uhusiano, Shamsa ambaye ni mama wa mtoto mmoja amesema hana tatizo kubeba ujauzito wa muimbaji huyo.
Shamsa aliyasema hayo alipoulizwa na jarida la Baabkubwa kama yuko tayari kumzalia Nay;
Aliongeza kuwa kuna kipindi waliachana lakini kwa sasa wamerudiana na wako karibu zaidi ya ilivyokuwa awali. Nay Wa Mitego ni baba wa watoto watatu ambaye kila motto ana mama yake, huku Shamsa Ford ni mama wa mtoto mmoja, Terry.“As long as ni wapenzi, tena tunaopendana sana, why not? If tumekubaliana for our future life”