Floyd Mayweather amemdunda Andre Berto kwa pointi kwenye pambano lao lililofanyika alfajiri ya leo kwa saa za Afrika Mashariki jijini Las Vegas kwenye ukumbi wa MGM Grand. Mayweather, 38, alishinda kwa pointi 120-108, 118-110 na 117-111.
“My career is over, that’s official, You’ve got to know when to hang them up. I’m close to 40 now. There’s nothing left to prove in the sport of boxing. Now I just want to spend time with my family.” alisema Mayweather.
Mayeweather amepigana mapambano 49 na amefanikiwa kushinda mapambano yote, hakuwahi kupigwa hata kwenye pambano moja!