Wiki hii tumepokea wimbo mpya wa Mabeste uitwao ‘Headache’, wimbo ambao ameonesha kipaji chake kingine cha kuproduce, sababu ameproduce mwenyewe mdundo. Ukiusikiliza utagundua uko tofauti na nyimbo zake zilizopita kama Dole, Sirudi tena na Baadae ambazo ni Hip Hop.
“Mimi si rapper tu peke yake ninaweza kufanya kila kitu ndani ya muziki, kwahiyo siwezi kuzuia hisia zangu ndani ya muziki endapo ninaona ninaweza kufanya.” Alisema Mabeste kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.
Akiongelea wasanii wa Hip Hop ambao huwa wanawachukulia tofauti rappers ambao huwa wanaamua kubadilika na kufanya aina tofauti ya muziki tofauti na Hip Hop amesema:
“Kwa artist ambaye anamchukia artist mwenzie ambaye amebadilika na kufanya kitu kingine ambacho ni kizuri pia ni ufupi wa akili tu, kwasababu kikubwa zaidi unachotakikana kufanya ni perferct , kitu ambacho kiko sahihi, ukishakuwa mwanamuziki huna tabaka la muziki unaweza ukafanya muzki wowote ilimradi ufanye vizuri, ukiuharibu ndio unakuwa umebugi.” Alimaliza Mabeste.
Usikilize wimbo huo hapa:
Habari hii pia inapatikana kwenye bongo5.com (source).
Usikilize wimbo huo hapa:
Habari hii pia inapatikana kwenye bongo5.com (source).