Mtalam III Mtalam III Author
Title: Msanii gani amefanya Verse kali kwenye wimbo mpya wa ‘DJ Choka - Stinga Li’?
Author: Mtalam III
Rating 5 of 5 Des:
Kama wewe ni shabiki mkubwa wa muziki wa Bongo flava utakuwa ushausikiliza vizuri wimbo mpya wa DJ Choka - Stinga Li uliotoka siku nne z...
Kama wewe ni shabiki mkubwa wa muziki wa Bongo flava utakuwa ushausikiliza vizuri wimbo mpya wa DJ Choka - Stinga Li uliotoka siku nne zilizopita. Wimbo huo ambao umetayarishwa na Pancho Latino na DJ Choka umewashirikisha wasanii mbalimbali.
Wasanii ambao wamesikika kwenye wimbo huu (kwa mtiririko wa verses zao) ni M-Rap, Dogo Janja, Pluto, Country Boy Weezy, Ms Rizzy na Young Dee. Uwepo wao umefanya wimbo huo umekuwa mzuri sana. Sasa swali ni kwamba, nani kafunika zaidi kuliko wengine?

Kama shabiki, nimeona Country Boy Weezy (amechana verse ya tatu) amefanya vizuri kwenye verse yake ndani ya wimbo huo kuliko rappers wote akifuatiwa na M-Rap (amechana verse ya kwanza). 

Mawazo yangu hayakupigwa sana kwani kuna baadhi ya mashabiki wanahisi Young Dee ndio kakimbiza wote (amechana verse ya mwisho) na Country Weezy na M-Rap ndo wanafata. Na wengine wafikiri tofauti na hivyo!

Young Dee huwa hakosei, lakini kwenye wimbo huu nahisi kama kachanganya mambo mengi kwenye verse yake kiasi cha kuifanya kutovutia kiviile (kwa upande wangu). Dogo Janja sijamkubali kabisa, Ms Rizzy anakuja vizuri na Pluto kafanya Chorus nzuri sana!

Sasa wewe sikiliza wimbo huo halafu sema mwenyewe nani kafanya verse kali kwenye wimbo huo wa DJ Choka, Stinga Li. Download au usikilize hapa:

Author

Advertisement

 
Top